Arc Hoteli

Morogoro, Tanzania

 Karibuni Arc hoteli iliyopo Morogoro , Tanzania .

 Arc hoteli imefunguliwa hivi karibuni, ni hoteli ya kisasa iliyo katika viwango vya kimataifa. Ipo pembezoni mwa mji wa Morogoro, 
 kama kilomita 2 toka   katikati ya mji, kandokando mwa barabara kuu ya Dar es Salaam kuelekea Dodoma au Zambia.

 Arc hoteli inatoa huduma nzuri ya vyumba vya kulala kwa mtu mmoja mmoja, wawili wawili au zaidi.  
 Vyumba vyake  vinatazama mandhari nzuri ya milima ya Uluguru.

 Mgahawa wa Arc hoteli unaoitwa 'Mikumi' hutoa huduma ya vyakula mbalimbali, vinavyotolewa ama ndani au nje kwenye eneo
 la wazi lenye hewa safi na upepo mzuri utokao milimani. Huduma katika mgahawa huu ni pamoja na kifungua kinywa, chakula
 cha mchana na jioni/usiku. Vyakula hivi ni vya mapishi ya Kiafrika, Kihindi, Kichina, Kimataifa,
 na vinginevyo vya kimataifa ambavyo hutayarishwa na wapishi wataalamu katika jiko lenye vifaa mbalimbali vya kisasa.
 
Huduma zitolewazo katika eneo lililowazi ni pamoja na huduma za baa iitwayo Wami-Mbiki'.

 Aidha, Arc hoteli ina ukumbi wa mikutano unaoitwa 'Udzungwa' wenye uwezo wa kupokea hadi watu 45 kwa ajili ya mikutano,
 semina au warsha.
                                                     
 

   KUPATA  NAFASI  MAWASILIANO  MALAZI  VYAMA NA KARAMU MAHALI ILIPO  UTALII: WA KIUTAMADUNI ENGLISH  


PICHA MBALIMBALI 
 

TAARIFA MUHIMU

 

Arc Hotel

Mfano bonyeza hapo chini na kupanua

Arc Hotel Arc Hotel Arc Hotel Arc Hotel Arc Hotel

Arc Hotel Arc Hotel Arc Hotel Arc Hotel

Arc Hotel Arc Hotel Arc Hotel  

Arc Hotel 

 


 Jinsi Ya Kutufikia

 Arc Hoteli ipo pembezoni mwa mji wa Morogoro, kama kilomita 2 toka katikati ya mji,
 kandokando ya barabara kuu ya Dar es Salaam kuelekea Dodoma au Zambia.

 Ipo mahali panapopendeza chini ya milima ya Tao la Mashariki na hasa karibu kabisa
 na milima ya Uluguru, Hoteli hii huonekana kwa urahisi upande wa kushoto katika
 barabara kuu ukitokea Dar es Salaam unapokaribia mji wa Morogoro kama
 inavyoonyeshwa katika ramani hapa chini.

 Bonyeza picha hapo chini kuona kubwa ukubwa eneo ramani kwa ajili ya Hotel Arc:

Arc Hotel map
1

 Ramani ya kina zaidi na maelekezo inapatikana kupitia Google.  ______________________  

 

 Visit us at:
 ARC HOTEL   TOURS

 

     Muda wa kutoka:  Saa 5 asubuhi
  Muda wa kuingia:  Saa 6 mchana
CREDIT CARDS ACCEPTED (no fees charged)
Visa Visa
Master Card Master Card
Eurocard Eurocard

HUDUMA KWA UJUMLA

Baa
Gari la kukodi
Baa ya kokteli(mchapalo)
Huduma za mikutano
Kifungua kinywa aina ya kimagharibi
Ukumbi wa chakula
Udobi
Huduma za Intaneti
Maegesho salama ya magari
Mgahawa
Huduma za vyumbani
Vyumba vyenye luninga
Huduma ya kuamshwa
 
HUDUMA ZA VYUMBANI
Kiyoyozi
Huduma za dobi
Mahali binafsi pa kuogea
Simu
Luninga
 

 SERA YA WATOTO
 Arc Hoteli inazikaribisha pia familia zenye 
 watoto. 
 Hoteli inao uwanja wenye michezo mizuri kwa
 watoto.

 

 
Lugha za mawasiliano
 
Kiingereza
 Kiswahili

 HUDUMA ZITOLEWAZO
 Burudani ya michezo kama vile mpiro wa miguu, muziki,
 sinema, "dokumentari" n.k. kupitia Luninga kubwa, DSTV,
 na sehemu maalumu ya kuoneshea burudani hizo.

 Gharama za Huduma
 Chumba mtu mmoja:       US$50
 Chumba cha watu wawili: US$65
 Apartment - suite:           US$130
 US$15 zinaongezeka kwa kila mtu mmoja
 anayeongezeka chumbani.
 Gharama hizi zinajumuisha mlo kamili wa asubuhi yaani
 kifungua kinywa.

 
 KUPATA NAFASI

  Sisi kuthibitisha booking yako ndani ya masaa 24.
  Kama huna uthibitisho, basi wasiliana nasi kwa
  barua pepe: info@archotel-tz.com

 
  MKUTANO WA VIFAA
  Mkutano chumba kwa siku: 150.000TZs (takriban 100US$)
  LCD / Multimedia Projector: 60.000TZs (takriban
40US$)
  Washiriki wa mkutano Package - 2 Chai / Kahawa na mapumziko
  vitafunwa na chakula cha mchana: 30.000TZs (takriban 20US$)
  ____________________________________________________

 Kwa Mawasiliano tuandikie:
 Arc Hotel
 P.O. Box 3112
 Morogoro, Tanzania

 Unaweza kupiga simu kama ifuatavyo:

Simu uwapo nchini: 023 2600250
Faksi uwapo nchini: 023 2600240
Simu uwapo nje ya nchi: +255 23 2600250
Faksi uwapo nje ya nchi: +255 23 2600240
Simu ya mkonomi: 0769 600240
          Simu ya mkononi uwapo nje: +255 769 600240
                                               Email: info@archotel-tz.com

Links kwa maelezo zaidi:
   *
Special rates for parties and banquets
   * Arc Hotel Brochure
  * Restaurant Special Menu
  * Wine Menu (Carte des Vins)

   *Comprehensive Menu
   * Safari programme